LATIFA HASSAN ALI

MKURUGENZI MSAIDIZI UENDESHAJI

HABARI ZA UENDESHAJI
VIDIO
Miaka 10 ya Mhe:Dr ALI mohammed Shein MKUU WA WILAYA YA KATI BI:HAMIDA MUSA KHAMIS akielezea Jinsi ilivojipanga jisi ya kukabiliana na Korona

MUUNDO WA IDARA YA MIPANGO UENDESHAJI FEDHA NA RASILIMALI WATU



IDARA YA MIPANGO UENDESHAJI FEDHA NA RASILIMALI WATU

Idara ya Mipango,Utawala, na Rasilimali Watu ni moja kati ya Idara sita za Halmashauri ya Wilaya ya kati ikiwa imejumuisha ndani yake Divisheni ya Utawala, Mipango, Fedha (MAPATO) na Rasilimali watu, ambapo Idara hii zinasimamia maslahi ya wafanyakazi wote wa Halmashauri,ikiwemo likizo,mafunzo,marekebisho ya mishahara na malipo yoyote wanayostahiki wafanyakazi kwa mujibu wa sheria. Pia inashughulikia ufuatiliaji na ukusanyaji wa mapato, vyombo vyote vya usafiri, na majengo ya Ofisi.

Dira

Kuwa na Wilaya mahiri yenye kuvutia kwa kupigania mfumo wa maisha ya maendeleo endelevu kutokana na kuwepo mazingira ya kipekee na kwa Wilaya mfano bora ndani ya Zanzibar na yenye kutambulika Ulimwenguni kote.

Dhamira

Kuandaa mazingira bora kwa wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya kati.

Mafanikio

Idara ya Uendeshaji Mipango na Fedha Imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika Baada ya kusimamia Dira yake na Kusimamia Dhamira yake

MAJUKUMU

  • Kupitia, kuimarisha, kusimamia na kuendesha utekelezaji wa Mipango na bajeti ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa
  • Kuimarisha na kushauri utekelezaji wa Miradi kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo katika mamlaka za serikali za Mitaa
  • Kutoa ushauri kuhusiana na taasisi za Mamlaka ya Serikali za Mitaa juu ya umuhimu wa kufanya shughuli za utafiti
  • Kuziendeleza Sekta binafsi kwenye shughuli za Maendeleo katika mamlaka ya serikali za Mitaa
  • Kusimamia na kutathmini utekelezaji wa Mipango ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa
  • Kusimamia mapato kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo iliokuwepo
  • Kuhakikisha Matumizi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa yanafanyika kwa mujibu wa Sheria ya fedha na Muongozo uliowekwa
  • Kutekeleza majukumu mengine yatakayotokezea kama itakavyopangwa na Uongozi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa