SAID MTAJI ASKARI
HALMASHAURI YA WILAYA KATI-ZANZIBAR
Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya kati-Zanzibar.Moja kati ya malengo yake kutoa huduma zilizobora kwa jamii inayoishi Wilaya ya kati na pia Wilaya ya kati imebarikiwa kua na Ardhi kubwa na yenye Rutba nyingi sana kwa ajili ya kilimo hvyo Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kati kutokana na Malengo yake kudhamamiria kuisaidia jamii ya Wilaya imeanzisha vitalu mbali mbali vinavyo patikanwa maeneo tofauti kama vile Afisi kuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kati(Dunga),Machui Karibu na Kambi ya Polisi FidForce(FFU)n.k vitalu hivi vinawasaidia wananchi wa wilaya ya kati katika upatikanaji wa miche mbali mbali Ambapo wananchi walio wengi huwendesha Maisha yao kupitia Kilimo
Wananchi wote wanakaribishwa katika kupatiwa huduma ya Miche
stage Tofauti inayo onyesha Miche Kuanzia stage ya awali kabla ya kuchipua kwa mbegu baada ya kuchipua na kukua kwa kiasi mpka kufikia katika hali ya muitwa michwa
Baadhi ya Vijana wanaoshiriki katika kujifunza fani ya ushoni ili kuweza kua na ujuzi na kuweza kujiajiri kuendesha Maisha yao
Ofisi ya Halmahauri imeweza kuanzisha sehemu ndogo ya kujifunza Fani ya Ushoni ili kuweza kuisaida Jamii katika kujipatia ujuzi huwo na Kuifanya jamii yenye kujitegemea na kuweza kujiajiri.
Kiwanda hichi cha matofali kimeweza kusaidia Baadhiya vijana waishio Ndani ya wilaya ya kati katika kupata ajira na kuweza kujishughulisha ili kuweza kupata kipato kwa ajili ya kuhudumia Familia zao
Wananchi wote Mnakaribishwa katika ununuzi wa Matofali kwa bei ilio Rahis na yenye kununulika.