SAID MTAJI ASKARI
HALMASHAURI YA WILAYA KATI-ZANZIBAR
MOHAMED SALUM MOHAMED
HALMASHAURI YA WILAYA KATI-ZANZIBAR
Halmashauri ya Wilaya ya Kati(HWK) ni moja kati ya Halmashauri 11 zilizoanzishwa kutokana na sheria za Serikali za mitaa ya namba 7 ya 2014.Halmashauri ya wilaya ya kati imo ndani ya mkoa wa kusini na imepakana na Wilaya ya kaskazini (B),wilaya ya kusini,wilaya ya maghrib (A) na bahari ya hindi kwa upande wa mashariki. Wilaya ya kati ina ukubwa wa kilomita za mraba 427.78 na ina idadi ya watu 76,346 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012,ambapo uchumi wake unachangiwa zaid na shughuli za kilimo,uvuvi pamoja na shughuli nyenginezo za kiuchumi. HWK ina majimbo matatu(3) nayo ni Uzin,Tunguu na Chwaka na pia ina Wadi nane(8)nayo ni Koani,Bambi,Kiboje,Tunguu,Ubago,Bungi,Cheju na Chwaka ,ambapo ina ndani yake mna Shehia(42). Kama ilivyo ainishwa katika Sheria ya serekali za mitaa ya Namba 7 na mwaka 2014 zifuatazo ni kazi za Halmashauri ya Wilaya ya Kati (HWK):- a)Kuunda,kupangilia na kusimamia utekelezaji wa mipango ya kiuchumi,kibiashara,viwanda na maendeleo ya jamii. c)kuunda sheria ndogo ndogo ambapo zitakua zanatumika ndani ya eneo lake husika. b)kuhakikisha ukusanyaji pamoja na utumiaji mzuri wa mapato ya Halmashauri.