MWENYEKITI HALMASHAURI YA WILAYA KATI-ZANZIBAR

SAID MTAJI ASKARI

HALMASHAURI YA WILAYA KATI-ZANZIBAR

KARIBU KATIKA UKURASA WA KITENGO CHA TEHAMA



KITENDO CHA TEHAMA

Ni kitengo ambacho kinashughulika na masuala ya uandishi wa taarifa , upigaji picha, kuandaa makala tofauti, uchambuzi wa habari pamoja na matukio mbali mbali yanayojitokeza na kuziwasilisha katika vyombo vya habari kwa lengo la kuwahabarisha wanajamii.

Dira

Kuwa na kitengo ambacho kinafanya kazi kwa umahiri, uweledi na usahihi bila ya kufanya upendeleo upande mmoja , na kuwa wawazi kwa wanajamii juu ya kila kinachoendelea katika kuwaletea maendeleo.

Dhamira

Kujenga imani kwa jamii juu ya habari zinazotolewa katika vyombo vya habari.

Mafanikio

  • Kitengo kimeweza kuitangaza Ofisi ya Halmashauri kwa kusambaza habari na matukio yanayotokea ndani ya Halmashauri, Wilaya na Taifa kwa ujumla.
  • Kufanyika Taasisi kuwa na muamko juu ya utoaji wa taarifa zao kupitia vyombo vya habari.
  • Tumekuwa kiunganishi baina ya jamii na Taasisi.
  • MAJUKUMU

  • Kuandaa taarifa za habari, mijadala, makala na kuyatoa katika vyombo vya habari.
  • Kuhifadhi na kuweka kumbukumbu za picha za kiofisi, jamii na za kitaifa.
  • Kupiga picha matukio mbali mbali.
  • Kuandaa vipeperushi vya kuelimisha,kufundisha na kuhabarisha katika masuala mbali mbali yanayojitokeza katika jamii.